Wataalamu wametahadharisha kwamba ubora wa mbegu za kiume miongoni mwa wanadamu umekuwa ushuka pakubwa, na kuathiri uzazi.
Hili linasababishwa sana na kula vyakula vya kisasa vyenye mafuta mengi na wanga pamoja na kutofanya mazoezi ya kutosha.
Athari zimejitokeza kwenye kiasi cha mbegu za uzazi anazotoa mwanamume na pia ubora wa mbegu zinazotolewa na uwezo wake kuogelea katika majimaji ya ukeni.
Wahudumu katika kliniki za masuala ya uzazi wanasema kiwango cha mbegu za uzazi zilizo bora kimekuwa kikishuka kwa takriban asilimia 2 kila mwaka.
Kushuka huku kwa kiwango cha mbegu za kiume kumeshuhudiwa miongoni mwa wanaofika kutaka kutoa mbegu za kutumiwa kuwatungisha mimba wanawake na wale wanaofika wakitaka wasaidiwe kuongeza kiwango cha ubora wa mbegu za uzazi ndipo waweze kutungisha mimba.
Matokeo ya utafiti huo yamewasilishwa katika kongamano la kila mwaka la Chama cha Matibabu ya Uzazi Marekani ambalo linaendelea mjini Denver, Colorado.
Kudhoofika pakubwa
Utafiti umeonyesha kwamba mbegu za kiume zimekuwa zikidhoofika pakubwa kiasi kwamba zinashindwa kuogelea kwenye majimaji ya mwanamke zikielekea kufikia yai kutungisha mimba.
Idadi ya wanaume wanaoomba usaidizi kutungisha mimba imeongezeka mara saba katika mataifa ya magharibi katika kipindi cha miaka 15 iliyopita.
Wataalamu wameeleza hali hiyo kuwa ya kuogofya.
Wataalamu wanaamini unene pamoja na mtindo wa maisha siku hizi wa kuketi vipindi virefu bila kufanya mazoezi kunachangia, pamoja na mabadiliko kwenye lishe na kemikali nyingi ambazo zipo kwenye mazingira.
Utafiti huo ulishirikisha wanaume 124,000 waliotembelea kliniki za uzazi Ulaya na Marekani, ambapo ilibainika kwamba ubora wa mbegu za uzazi unashuka kwa 2% kila mwaka.
Chanzo na BBC.
Title :
Utafiti: Wasiwasi kutokana na kushuka kwa kiwango na ubora wa mbegu za kiume Ulaya na Marekani
Description : Wataalamu wametahadharisha kwamba ubora wa mbegu za kiume miongoni mwa wanadamu umekuwa ushuka pakubwa, na kuathiri uzazi. Hili linasab...
Rating :
5