Mshambulizi wa timu ya taifa ya soka ya Kenya, Harambee Stars, Michael Olunga anayeichezea klabu ya Djurgardens IF ya Sweden, ameendeleza fomu yake nzuri katika ligi kuu ya taifa hilo kwa kufunga magoli mawili na kuiwezesha timu yake kuilaza Malmo Fc inayoshikilia nafasi ya pili 3-1.
Mabao hayo yalimwezesha Olunga, aliyehama mabingwa wa ligi ya soka ya Kenya, Gor Mahia, kuongeza idadi yake ya magoli hadi saba na kushikilia nafasi sawa katika orodha ya wafungaji bora wa klabu hiyo.
Ushindi huo uliipa klabu ya Djurgardens ushindi wa tatu mfululizo katika mechi zake za hivi karibuni.
Timu hiyo ina alama shikilia nafasi ya kumi na moja baada ya kucheza mechi 22 ikiwa na alama 28.
Kufikia sasa, Olunga amecheza jumla ya mechi 20 ambapo alianza mechi 12 kati ya mechi hizo.
Kocha wake, Mark Dempsey, amemsifu mfungaji huyo na kueleza kuwa bidii yake imemwezesha kunawiri.
"Anajituma mwenyewe na ni vyema kwa sababu inaisaidia timu''.
Djurgardens itachuana na AIK Fotboll kwenye debi ya Stockholm itakayochezwa jumatano katika mechi ya ligi.
Title :
Mkenya Michael Olunga afunga mabao mawili ligini Sweden
Description : Mshambulizi wa timu ya taifa ya soka ya Kenya, Harambee Stars, Michael Olunga anayeichezea klabu ya Djurgardens IF ya Sweden, ameende...
Rating :
5