Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametoa Sh125 milioni kwa mwenzake wa Tanzania Dkt John Magufuli kama rambirambi kufuatia mkasa wa kuzama kwa kivuko cha MV Nyerere mwezi jana.
Watu 228 walifariki na wengine wengi kujeruhiwa katika mkasa huo uliotokea tarehe 20 kivuko cha MV Nyerere kilipokuwa safariki kuelekea kisiwa cha Ukara kutoka kisiwa cha Ukerewe.
Mchango huo wa Rais Kenyatta umewasilishwa kwa Rais Magufuli na balozi wa Kenya nchini tanzania Dkt Dan Kazungu aliyekutana na kufanya mazungumzo naye ikulu Dar es Salaam.
Rais Magufuli amemshukuru rais Kenyatta na akaahidi kwamba fedha zilizotolewa na Rais Kenyatta zitatumiwa kuwasaidia wananchi wa visiwa vya Ukerewe, ikiwa ni pamoja na kuchangia kujenga hospitali ya hadhi ya wilaya.
Adokeza kwamba huenda wodi moja katika hospitali hiyo ikapewa jina la kiongozi huyo wa Kenya.
"Mwambie Mhe. Rais kuwa nashukuru sana, tulipanga fedha tulizopata tjenge wodi za wagonjwa lakini sasa tumeamua tujenge hospitali kubwa yenye hadhi ya wilaya," amesema Rais Maufuli.
"Na kwa mchango huu, tunaweza kuamua wodi moja tukaiita Wodi ya Kenyatta."
Title :
MV Nyerere: Kenyatta atoa Sh125m kwa Watanzania kama rambirambi mkasa wa kivuko
Description : Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametoa Sh125 milioni kwa mwenzake wa Tanzania Dkt John Magufuli kama rambirambi kufuatia mkasa wa kuzama kwa...
Rating :
5