Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewaonya wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa na Wakurugenzi wote nchinikujifunza kutumia vizuri fedha za serikali.
Rais Magufuli ameyasema hayo Jumatatu hii, wakati wa uzinduzi wa nyumba 50 za wahudumu wa afya, zilizojengwa na Taasisi ya Mkapa Foundation.
“Nitoe wito kwa Wakuu wa Wilaya na wakuu wa Mikoa na Wakurugenzi wote Tanzania tujifunze kutumia vizuri fedha za serikali kwasababu tatizo tulilo nalo katika Halmashauri zetu ni matumizi mabaya ya fedha za Serikali unaweza kuta Waziri Ummy anahangaika kutafuta hizo fedha pasitokee mchwa wakula hizo fedha madawa yatumwe alafu watu kila siku waende hospitalini waaseme madawa hayapo hayajatumwa na serikali. Nawaomba viongozi wenzangu tubadilike,”
Title :
Rais Magufuli atoa wito kwa wakuu wa Mikoa na Wilaya
Description : Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewaonya wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa na Wakurugenzi wote nchini kuj...
Rating :
5