Serikali itaunda tume ya uchunguzi itakayohusisha timu ya wataalamu na vyombo ya dola, kuhakikisha chanzo cha ajali kinatambulika.
Jumla ya miili 224 imeopolewa kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Waziri wa uchukuzi mhandisi Isack Kamwelwe.
Maafisa wote wanaohusika na uendeshaji wa kivuko wamekamatwa na wanahojiwa kwa uchunguzi.
Mazishi yataendelea kufanyika pale miili ikipatikana na Waziri mkuu ataendelea kubaki kisiwani Ukara, hasa katika kushiriki mazishi ya wale ambao hawatatambuliwa na ndugu zao.
Karibu miili 9 ya waathiriwa kwa ajali ya MV Nyarere ambayo ilizama Alhamisi inazikwa leo kweny makaburi mengi ya pamoja katika fukwe za kisiwa cha Ukara, hatua chache kutoka eneo ajali ilitokea.