Tume ya Uchaguzi nchini Rwanda , imemtangaza Rais Paul Kagame kuwa mshindi wa kiti cha Uraisi katika uchaguzi uliofanyika jana.
Rais Kagame ambaye amekuwa madarakani kwa miaka kumi na saba, ameshinda nafasi ya Uraisi kwa kupata asilimia 98 ya kura zilizohesabiwa baada ya uchaguzi huo.
Uchaguzi huyo ulihusisha chama cha Rais Paul Kagame (Rwandan Patriotic Front )RPF, chama Green Party cha Frank Habineza na Philippe Mpayimana, mgombea huru.
Baada ya matokeo hayo wapinzani wa Kagame wamelalamika kuwa wafuasi wao walisumbuliwa wakati wa kampeni hali iliyopelekea kutokuwepo kwa wapiga kura wa kutosha jambo ambalo limepigwa na chama tawala.
Title :
Rais Kagame kuongoza Rwanda
Description : Tume ya Uchaguzi nchini Rwanda , imemtangaza Rais Paul Kagame kuwa mshindi wa kiti cha Uraisi katika uchaguzi uliofanyika jana. ...
Rating :
5