Baada ya ukimya wa muda mrefu msanii wa Bongo Flava, Keisha ametangaza ujio mpya na kusema ujio wake hauna kiki.
Keisha amesema mashabiki wake wachagua wenyewe kama wanataka muziki mzuri au wanataka muziki wa kiki.
“Kama wanataka muziki mzuri watapata, kama wanataka muziki wa kiki wafuate huko, mimi sifanyi muziki kiki,” Keisha ameimbia PUSH TALENT YA NTAMBA TV na kuongeza.
“Siwezi kufanaya muziki wa kiki kwa sababu mimi ni msanii halisi, sibebwi kama nimeweza kupita kipindi kile ina maana una kipaji halisi,” amesema.
Katika kusisitiza msimamo wake amemtolea mfano msanii Aslay kwa kusema anafanya muziki mzuri na watu wanamuelewa bila hata ya kiki, “katoa nyimbo tatu kali bila kiki na zote unasikiliza unaoana nyimbo ni kali, kwa hiyo muziki mzuri upo,” amesema Keisha.
Title :
Keisha: Siwezi kufanya muziki wa kiki, ‘ampa tano Aslay’
Description : Baada ya ukimya wa muda mrefu msanii wa Bongo Flava, Keisha ametangaza ujio mpya na kusema ujio wake hauna kiki. Keisha amesema mash...
Rating :
5