Kwa mara nyingine tena, Rais BARACK OBAMA
amesema, mgombea wa kiti cha urais nchini humo kupitia chama cha
REPUBLICAN, DONALD TRUMP hafai
OBAMA asema TRUMP hafai kuwa Rais
Kwa mara nyingine tena, Rais BARACK OBAMA wa MAREKANI
amesema, mgombea wa kiti cha urais nchini humo kupitia chama cha
REPUBLICAN, DONALD TRUMP hafai kuwa rais wa nchi hiyo wa vile amekuwa
akifanya vitu vingi vya kusikitisha.
Akizungumza nchini SIGNAPORE, OBAMA amesema uwezo mdogo wa TRUMP
kujua na kuyafanyanyia tathimini masuala ya mashariki ya kati na masuala
yanayohusu ustawi wa taifa la MAREKANI, unadhihirisha jinsi asivyoweza
kuongoza nchi.
Kwa mara nyingine TRUMP amejichanganya baada ya kuikashifu familia
moja ambayo, mmoja wa wanafamilia wake, alitoa muhanga maisha yake kwa
ajili ya ustawi wa watu wa MAREKANI, na kuhesabika kuwa ni mmoja wa
mashujaa wa taifa hilo.
Wapinzani wa TRUMP pia walimshutumu kuwa ni kiongozi muoga, baada ya
kukimbia jeshi kwa visingizio vya ugonjwa wakati wa vita vya VIETNAM.
August 3, 2016
NYAMBONA MASAMBA
Title :
RAIS OBAMA ADAI TRUMP HAFAI KUWA RAISI WA MAREKANI.
Description : Kwa mara nyingine tena, Rais BARACK OBAMA amesema, mgombea wa kiti cha urais nchini humo kupitia chama cha REPUBLICAN, DONALD TRUMP hafa...
Rating :
5