Rais MAGUFULI apokea taarifa ya ujenzi wa kiwanda cha LNG
Rais
Dkt. John Pombe Magufuli amepokea taarifa ya maendeleo ya mradi mkubwa
wa ujenzi wa kiwanda cha kusindika gesi asili -LNG Plant
Rais
Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwakilishi wa Kampuni ya
Mafuta ya Stat Oil ya Norway, Bw. Oystein Michelsen kabla ya kupokea
taarifa ya maendeleo ya mradi mkubwa wa ujenzi wa kiwanda cha kusindika
gesi asili (LNG Plant)
Rais Dkt. John Pombe Magufuli amepokea taarifa ya maendeleo
ya mradi mkubwa wa ujenzi wa kiwanda cha kusindika gesi asili -LNG Plant
kinachotarajiwa kujengwa katika eneo la Likon'go, Mchinga Mkoani Lindi.
Mwakilishi Mkazi wa Kampuni ya Statoil ya nchini Norway ambayo ni
moja ya Kampuni zitakazowekeza katika mradi huo Oystein Michelsen
amemueleza Rais Magufuli kuwa ujenzi wa kiwanda hicho unatarajiwa
kugharimu Dola za Kimarekani Bilioni 30 sawa na zaidi ya Shilingi
Trilion 65 za Kitanzania na kwamba uzalishaji unatarajiwa kuchukua muda
wa zaidi ya miaka 40 baada ya kuanza.
Oystein Michelsen amebainisha kuwa Serikali ya Norway ina dhamira ya
dhati ya kuhakikisha mradi huo unatekelezwa kwa manufaa ya pande zote na
ameomba Serikali ya Tanzania iendelee kutoa ushirikiano ili kufanikisha
ujenzi wa kiwanda hicho.
Kwa upande wake Rais Magufuli amemuhakikishia Mwakilishi huyo wa
kampuni ya Statoil kuwa Serikali ya Tanzania ipo tayari kuhakikisha
mradi unafanikiwa na ameitaka Wizara ya Nishati na Madini kupitia
Shirika la Maendeleo ya Petroli –TPDC kushirikiana na wadau kutoka
Wizara nyingine kuharakisha mchakato wa kuanza kwa ujenzi wa kiwanda
hicho.
Dkt. Magufuli amesema mradi huo unatarajiwa kuzalisha ajira kwa idadi
kubwa ya watanzania na utaiwezesha serikali kupata mapato kupitia tozo
mbalimbali, na hivyo kutumika kuimarisha huduma za kijamii zikiwemo
elimu, afya, maji na miundombinu.
Pamoja na Statoil kampuni nyingine zinazoshiriki katika uwekezaji wa mradi huo ni Shell, Exxon
Title :
Rais MAGUFULI apokea taarifa ya ujenzi wa kiwanda cha LNG
Description : Rais MAGUFULI apokea taarifa ya ujenzi wa kiwanda cha LNG Rais Dkt. John Pombe Magufuli amepokea taarifa ya maendeleo ya mradi...
Rating :
5