Mganga mkuu wa DODOMA aagizwa kutafuta eneo kwa wajawazito
Siku
mbili baada ya kituo cha TBC1 kutangaza habari kuhusu msongamano wa
wajawazito katika kituo cha CHIKANDE kilichoko katika Hospitali ya Rufaa
ya Mkoa wa DODOMA
Mkuu wa mkoa wa DODOMA JORDAN RUGIMBANA
Siku mbili baada ya kituo cha TBC1 kutangaza habari kuhusu
msongamano wa wajawazito katika kituo cha CHIKANDE kilichoko katika
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa DODOMA, Mkuu wa Mkoa huo, JORDAN
RUGIMBANA amemwagiza Mganga Mkuu wa Mkoa kutafuta eneo mbadala kwa ajili
ya utoaji wa huduma bora.
RUGIMBANA amesema hali ya sasa hairidhishi na hivyo viongozi wa
hospitali ya rufaa ya mkoa wa DODOMA watafute eneo rafiki kwa wakinamama
wanaosubiri kujifungua.
Kituo cha chikande kinahudumia akina mama wajawazito kutoka katika
wilaya za mkoa wa Dodoma ambao wanahitaji huduma za kujifungulia katika
hospitali ya rufaa.
Title :
MGANGA MKUU WA DODOMA AOBWA KUTAFUTA ENEO LA WAJAWAZITO
Description : Mganga mkuu wa DODOMA aagizwa kutafuta eneo kwa wajawazito Siku mbili baada ya kituo cha TBC1 kutangaza habari kuhusu msongam...
Rating :
5