Rais MAGUFULI atembelea wagonjwa
Rais Dkt. John Pombe Magufuli amewatembelea na kuwajulia hali Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza
jambo na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai
nyumbani kwake Sala sala jijini Dar es Salaam alipokwenda kumjulia hali
Rais Dkt. John Pombe Magufuli amewatembelea na kuwajulia
hali Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai na
Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri Mkuu
Mstaafu John Malecela Jijini Dar es Salaam.
Pamoja na kuwajulia hali, Rais Magufuli aliyeongozana na Mkewe Mama
Janeth Magufuli amewaombea kwa Mwenyezi Mungu wapone na kupata nguvu
haraka ili waweze kuendelea na majukumu yao ya kawaida katika ujenzi wa
Taifa.
Akizungumza na Rais Magufuli nyumbani kwake Salasala Jijini Dar es Salaam spika wa Bunge Job Ndugai amemshukuru Rais
|
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli akimjulia hali Waziri Mkuu mstaafu John Samuel malecela
ambaye anapata matibabu jijini Dar es salaam, nyuma ni mke wa Rais Mama
Janeth Magufuli Agosti 16,201 |
Magufuli kwa kumtembelea, kumjulia hali na kufuatilia kwa ukaribu
wakati wote alipokuwa akipata matibabu nchini India hadi aliporejea hapa
nchini.
Ndugai amesema kwa sasa anaendelea vizuri na anaweza kufanya kazi ila anawaomba watanzania waendelee kumuombea.
Kwa upande wake Makamu wa Rais Mstaafu na Waziri Mkuu Mstaafu John
Malecela pamoja na kumshukuru Rais Magufuli na Mkewe Mama Janeth
Magufuli kwa kumtembelea amesema afya yake inazidi kuimarika na pia
amewashukuru Madaktari wanaompatia matibabu.
Title :
RAIS. JP MAGUFULI ATEMBELEA WAGONJWA
Description : Rais MAGUFULI atembelea wagonjwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli amewatembelea na kuwajulia hali Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa ...
Rating :
5