Makamu wa Rais SAMIA SULUHU HASSAN
amewahimiza wananchi wa Tanzania Bara na Zanzibar kuunga mkono jitihada
zinazofanywa na serikali
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akizungumza wakati anahitimisha kilele cha sikukuu ya WAKIZIMKAZI
Makamu wa rais SAMIA SULUHU HASSAN amewahimiza wananchi wa
Tanzania Bara na Zanzibar kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
katika mapambano dhidi ya rushwa, na ufisadi ili kukomesha tabia hiyo
ambayo inarudisha nyumba maendeleo ya wananchi.
Makamu wa Rais ametoa kauli hiyo
wakati anahitimisha kilele cha sikukuu ya WAKIZIMKAZI katika kijiji cha KIZIMKAZI MKUNGUNI wilayani ya Kusini Unguja – ZANZIBAR.
Aidha makamu wa Rais amewahakikishia wakazi hao kuwa serikali
itaendelea kuchukua hatua kali kwa watendaji wanaorudisha nyuma
maendeleo ya wananchi ikiwemo ubadhirifu wa fedha za umma ili kukomesha
tabia hiyo.
Mama SAMIA ni mwasisi wa sikukuu hiyo ambayo inatumiwa na wakazi wa
maeneo hayo kufanya michezo mbalimbali ya jadi pamoja na kujadili na
kuweka mipango na mikakati ya maendeleo kwa ushirikiano na viongozi wao
Title :
MAKAMU WA PILI AHIMIZA JITIHADA SERIKALINI
Description : Makamu wa Rais SAMIA SULUHU HASSAN amewahimiza wananchi wa Tanzania Bara na Zanzibar kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali ...
Rating :
5