Moja kati ya watu anaowaheshimu rapa Chidi Benz, ni Babutale, kwasababu
meneja huyo wa Diamond ametumia fedha nyingi hadi sasa kwaajili yake.
“Huwezi amini mpaka sasa hivi ninavyoestimate kwamba Tale anaweza akawa
ametumia kama milioni 45, 50, 60. Sio kuwekeza, vitu ambavyo vimefanyika
tayari, lakini sijasaini wala nini,” alisema Chidi kwenye kipindi cha
The Playlist cha Times FM.
“Tale anachokifanya anaonesha kwamba ‘nia yangu mimi sio lazima tukabane
kwenye suala la hela, nia yangu wewe uwe sawa, uwe okay, uwe poa.’
Kwahiyo ina maana mimi sijasaini lakini nachukulia kwamba yeye aone
kusaini inawekana nikasaini ukaniletea mkataba wa miaka miwili but mimi
sasa naishi na wewe kabisa,” aliongeza.
Chidi anadai kuwa anamchukulia Tale kama familia yake.
“Kwasababu hata sasa hivi nakaa kwake, bado niko kwao so yaani kwahiyo
hata ukija mkataba labda aniandikie miaka 20 kwamba haina maana.”
Tale alimsaidia rapper huyo kumsaidia kuepukana na uraibu wa madawa ya
kulevya ikiwa pamoja na kumpeleka rehab na baada ya kutoka kuingia
studio kurekodi nyimbo mpya. Hivi karibuni aliachia wimbo wake mpya
‘Chuma’ aliomshirikisha Raymond.
Title :
CHIDI BENZI AKIRI KUENDELEA KUISHI KWA BABU TALE
Description : Moja kati ya watu anaowaheshimu rapa Chidi Benz, ni Babutale, kwasababu meneja huyo wa Diamond ametumia fedha nyingi hadi sasa...
Rating :
5