Meneja wa mwanamuziki wa kimataifa Diamond Platnumz, Hamis Tale Tale
maarufu kwa jina la ‘Babu Tale’ hivi sasa yupo mikononi mwa polisi
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.
Babu Tale amekamatwa leo na kufikishwa mahakamani hapo ili ajieleze ni
kwa nini asifungwe kwa kushindwa kutekeleza hukumu ya Mahakama
iliyomwamuru alipe fidia ya Sh250 milioni kwa makosa ya kuvunja sheria
ya Hakimiliki.
Babu Tale anatakiwa alipe fedha hizo kutokana na kuvunja mkataba kati
yake na Shekhe Mbonde, kwa kuuza na kusambaza nakala za mawaidha (DVDs)
bila ridhaa ya shekhe huyo, jambo ambalo ni kinyume na haki miliki
Title :
BABU TALE AWEKWA CHINI YA ULINZI MKALI
Description : Meneja wa mwanamuziki wa kimataifa Diamond Platnumz, Hamis Tale Tale maarufu kwa jina la ‘Babu Tale’ hivi sasa yupo mikononi ...
Rating :
5