Mwanamuziki wa Nigeria anayeunda kundi la Psquare Peter Okoye ameomba msamaha kwa washabiki kufuatia ugomvi na kaka yake.
Kupitia video iliyosambaa katika mitandao ya kijamii amesema timu nzima ya Psquare kwa sasa imerudi tena pamoja.
Akiwa
amevalia kofia ndani ya gari, video hiyo inamuonesha Okoye ni mwenye
kujuta, akisema kuwa anabeba jukumu kwa yote yaliyotokea.
Peter
alikuwa na uhasama na pacha wake Paul, ambaye ndiye amekuwa akiimba naye
kwa zaidi ya muongo mmoja, hali iliyofanya kugawa kundi hilo.
Kulikuwa na dalili kwamba utengano wao huo unahatarisha mafanikio ya mapacha hao.
Peter na Paul ambao wanapiga muziki wa hiphop wametoa nyimbo nyingi zilizovuma ndani ya Nigeria na nchi nyingine za Afrika.
Title :
PETER WA PSQUARE ARUDI KUNDINI RASMI AOMBA RADHI MASHABIKI.
Description : Mwanamuziki wa Nigeria anayeunda kundi la Psquare Peter Okoye ameomba msamaha kwa washabiki kufuatia ugomvi na kaka yake. Kupitia vi...
Rating :
5