Katika habari za usajili, timu ya RUBIN KAZAN
imekamilisha usajili wa kiungo ALEX SONG kwa uhamisho wa bure kwa
mkataba wa mitatu kutoka kwa miamba wa soka nchini HISPANIA FC
BARCELONA.
ALEX SONG
SONG aliitumikia klabu ya wagonga nyundo wa London WEST HAM
UNITED msimu uliopita kwa mkopo baada ya kukosa nafasi ya kudumu katika
kikosi cha FC BARCELONA.
Nayo Klabu ya SOUTHAMPTON imemsajili golikipa ALEX MCCARTHY kwa mkataba wa miaka mitatu kutoka timu ya CRYSTAL PALACE.
MCCARTHY, alicheza michezo saba msimu uliopita akiwa na klabu yake ya CRYSTAL PALACE.
Huu ni usajili wa tatu kwa timu hii maarufu kwa jina la Watakatifu wa
SOUTHAMPTON baada ya kuwasajili NATHAN REDMOND na PIERRE-EMILE
HOJBJERG.
Nae beki STEVEN TAYLOR amejiunga na timu ya PORTLAND TIMBERS, inayoshiriki ligi ya kuu ya Marekani akitokea NEWCASTLE UNITED.
Beki huyu amekaa kwenye klabu ya NEWCASTLE UNITED kwa muda mrefu tangu akiwa na umri wa miaka 21 na ameichezea michezo 268.
Title :
ALEX SONG ASAJILIWA NA UBIN KAZAN IKIMBIA WEST HUM UNITED
Description : Katika habari za usajili, timu ya RUBIN KAZAN imekamilisha usajili wa kiungo ALEX SONG kwa uhamisho wa bure kwa mkataba wa mitatu kutoka...
Rating :
5