MO aipa SIMBA FC Milioni Mia
Mwanachama
wa klabu ya AZAM MOHAMED DEWJI ametoa shilingi MILIONI MIA kwa klabu ya
SIMBA ili kusaidia zoezi zima la usajili wa klabu ya SIMBA ambao
wanahitaji fedha zaidi za kusajili wachezaji wataoisaidia timu hiyo
kufanya vizuri katika ligi
Mohamed
Dewji akimkabidhi mfano wa hundi sh. milioni 100 Rais wa Simba SC,
Evans Aveva kama mchango wake katika usajili wa klabu hiyo
Akizungumza wakati wa kukabidhi hundi hiyo MOHAMED DEWJI
amesema ametoa MILIONI MIA kwa lengo la kusaidia mchakato wa usajili
huku Rais wa SIMBA EVANS AVEVA akisema katika fedha hizo watampata
mchezaji kutoka IVORY COAST.
Bado siku chache kabla ya dirisha la usajili kufungwa hivyo uongozi
wa SIMBA umesema utatumia muda uliobaki kukamilisha usajili wa wachezaji
wake huku ikiwa bado inahitaji fedha zaidi ya MILIONI MIA TATU
kukamilisha usajili.
Title :
MO AIPA SIMBA FC MILIONI MIA
Description : MO aipa SIMBA FC Milioni Mia Mwanachama wa klabu ya AZAM MOHAMED DEWJI ametoa shilingi MILIONI MIA kwa klabu ya SIMBA ili kusaidia zoe...
Rating :
5