Kulitokea kizaza katika kituo kimoja
cha polisi nchini Kenya askari polisi aliyeacha kazi mwenyewe alipovua
nguo na kusalia uchi wa mnyama akijaribu kumshinikiza inspekta mkuu
jenerali wa polisi Joseph Boinnet kumrejesha kazini.
Afande huyo alivua nguo na kujifunika gunia katika kituo cha polisi cha Lang’ata jijini Nairobi mapema leo asubuhi.
Afisa
huyo anadaiwa kuwa aliacha kazi mwenyewemiezi 6 iliyopita kwa
madhumuni ya ''kuendeleza kazi ya bwana'' ama kuhubiri injili, hata
hivyo 'kazi'' haikushika kasi ipasavyo na mara akajipata anadaiwa kope
si zake.
Aliona kheri arejee kazini kuomba msamaha mkubwa wake lakini hilo halikumsaidia kupata unga.
Maafisa wa polisi walimkamata na kumweka rumande.
Title :
POLISI.AVUA NGUO KWA KUTAKA KURUDISHWA KAZINI KENYA.
Description : Kulitokea kizaza katika kituo kimoja cha polisi nchini Kenya askari polisi aliyeacha kazi mwenyewe alipovua nguo na kusalia uchi wa mn...
Rating :
5