Manchester City, wakicheza mechi yao
ya kwanza ya kujiandaa kwa msimu mpya chini ya meneja mpya Pep
Guardiola, wamechapwa bao moja kwa bila na klabu ya zamani ya meneja
huyo Bayern Munich.
City walifungwa bao moja na Erdal Ozturk wa Bayern, ambao kwa sasa mkufunzi wao ni Carlo Ancelotti.
Wachezaji wengi nyota hawakucheza mechi hiyo kwani bado wanapumzika baada ya kushiriki Euro 2016 na Copa America.
Guardiola alichezesha wachezaji 12 wa timu ya vijana, mechi hiyo iliyochezewa Allianz Arena.
Mlinda lango wao alikuwa Angus Gunn, mwanawe mchezaji nyota wa zamani wa Norwich Bryan.
City sasa wataelekea Uchina ambapo watacheza dhidi ya Manchester United siku ya Jumatatu.
Watasafiri na Sergio Aguero, David Silva, Nolito, Raheem Sterling na Joe Hart.
Kikosi cha Manchester City kipindi cha kwanza:
Caballero, Maffeo, Adarabioyo, Kolarov, Angelino, Fernando, Fernandinho, Zinchenko, Barker, Iheanacho, Navas
Kipindi cha pili:
Gunn, Maffeo, Adarabioyo, Kolarov, Angelino, Clichy, Fernando, Fernandinho, Delph, Bony, Navas
Title :
GUADIOLA, APOKEA KICHAPO KUTOKA BAYEN MUNICH
Description : Manchester City, wakicheza mechi yao ya kwanza ya kujiandaa kwa msimu mpya chini ya meneja mpya Pep Guardiola, wamechapwa bao moja kwa...
Rating :
5