Hatma ya mshindi wa kombe la dunia
Bastian Schweinsteiger katika klabu ya Manchester United haijulikani
kufuatia kuajiriwa kwa kocha Jose Mourinho .
Mourinho tayari amefanya usajili wa wachezaji watatu na sasa anamuandama kiungo wa kati wa Juventus Paul Pogba.
Schweinsteiger mwenye umri wa miaka 31,anaonekana kuwa mmoja wa wachezaji tisa ambao huenda wakaihama klabu hiyo.
Kiungo huyo wa kati ambaye ametangaza kustaafu katika soka ya kimataifa
alifanya mazoezi pekee wakati ambapo wenzake walifanya zoezi pamoja kwa
mara ya kwanza.
Washambuliaji Adnan Januzaj,Will Keane na James
Wilson ,kiungo wa kati Andreas Pereira na mabeki Cameron
Borthwic-Jackson,Tim Fosu Mensah,Tyler Blackett na Paddy McNair pia
wameripotiwa kuondoka ijapokuwa wengine wataondoka kwa mkopo.
Kati ya wachezaji hawa hakuna hata mmoja aliyechaguliwa katika kikosi
cha wachezaji 23 kwa mechi ya kirafiki siku ya Jumamosi dhidi ya
Galatasaray mjini Gothenburg.
Title :
HATMA YA SCHWEINSTEIGER MAN U BADO SINTOFAHAMU
Description : Hatma ya mshindi wa kombe la dunia Bastian Schweinsteiger katika klabu ya Manchester United haijulikani kufuatia kuajiriwa kwa kocha Jo...
Rating :
5