KUNA tetesi kuwa mwanadada asiyekauka kwenye ‘media’ ambaye pia anafanya
Muziki wa Bongo Fleva, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ amemuundia jeshi
aliyekuwa mwandani wake Naftari Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ kuhakikisha
linamfanyia fujo mara kwa mara ili asiishi kwa amani wala kufanya vizuri
kimuziki.
Baada ya tetesi hizo kuenea, Burudani Mwanzo Mwisho (BMM), lilimvutia
waya Shilole ili kufungukia madai hayo na alipopatikana ‘aliwaka’ na
kudai hataki kumzungumzia Nuh wala hajui lolote kuhusu madai hayo.
“Sihitaji kabisa kuzungumza ishu yoyote kuhusu huyo mtu, niacheni kabisa
na wala sifahamu lolote kuhusu madai hayo,” alisema Shilole.
Alipotafutwa Nuh, alisema amesikia ishu hiyo lakini anaamini haitafanikiwa kwani Mungu anampigania.
Title :
SHILOLE AMUUNDIA KAMATI NUH MZIWANDA
Description : KUNA tetesi kuwa mwanadada asiyekauka kwenye ‘media’ ambaye pia anafanya Muziki wa Bongo Fleva, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ amem...
Rating :
5