SIKU chache baada ya kufikishwa katika kituo maaulum cha kusaidia
waathirika wa dawa za kulevya Bagamoyo Sober House, meneja wa kituo
hicho, Godwin Msilo ameeleza mazito ya mrembo huyo sambamba na maendeleo
yake kwa ujumla.
Ray C alifikishwa kwenye kituo hicho Ijumaa iliyopita baada ya kukamatwa
na polisi maeneo ya Kinondoni jijini Dar akifanya vurugu baada ya
kudaiwa kuzidiwa na ulevi wa madawa ya kulevya.
Akizungumza na wanahabari wetu Jumanne iliyopita katika kituo hicho,
meneja huyo alisema kilichomponza Ray C hadi arudie kwenye matumizi ya
madawa ya kulevya kwa mara ya pili baada ya awali kupatiwa tiba katika
Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar, ni aina ya tiba hiyo kwani ilikuwa
ikimpa mwanya wa kurudia kwenye matumizi ya madawa hayo.
Alisema, wao wanaamini tiba sahihi ya mtu aliyetopea kwenye madawa ya
kulevya ni muathirika kufikishwa Sober House kwani wao wanamfanya
muathirika asiweze kukutana na watu wengine wanaoweza kumshawishi arudie
madawa hayo hatari.
Kwa mujibu wa meneja huyo, kitendo cha kumpa dawa pekee (methadone) za
kumtibu muathirika wa madawa ya kulevya kisha kumuacha arejee mtaani ni
tatizo kubwa lililofanyika awali kwani kilimpa mwanya mrembo huyo
kujichanganya na watumiaji wa madawa ya kulevya mitaani.
“Huwezi kumtibu mtu kwa kumpa dawa halafu ukamwacha muathirika arudi
nyumbani, utakuwa umemjenga vipi kisaikolojia? Kuna haja ya kumchukua
muathirika kumuweka sehemu katika kituo kama hiki, anapata dawa,
akishapata dawa, anapata elimu anakutana na madaktari wa afya ya akili,
anakutana na madaktari wa saikolojia, wanamjenga kisaikolojia.
“Huwezi kumwacha tu, arudi nyumbani. Hujui anakula vipi, anaishije, hiyo
haipo. Hivi vitu vinataka mtu ajitoe kwelikweli, apate tiba sahihi kwa
kujengwa vizuri ili hata akirudi uraiani, atakuwa na uwezo mzuri wa
kujisimamia mwenyewe kutokana na elimu atakayokuwa ameipata,” alisema
Msilo.
Kuhusu maendeleo ya Ray C ambaye hadi Jumanne iliyopita alikuwa
ametimiza takriban siku tano kituoni hapo, meneja huyo ambaye pia
aliwahi kuwa muathirika wa madawa ya kulevya kabla ya kutibiwa, alisema
mrembo huyo kwa sasa anaendelea vizuri.
Yeah! Ameanza vizuri tiba, anaendelea vizuri kwa kweli. Naamini kadiri
anavyoendelea atakuwa vizuri zaidi. Kuna mabadiliko makubwa ameanza
kuyaonesha,” alisema Msilo huku akidai muda wa kuwepo kwenye nyumba hiyo
utategemeana na jinsi Ray C atakavyoonesha kupona.
Akijizungumzia yeye kama mfano wa watumiaji waliotopea na kisha
kutibiwa, Msilo alisema licha ya kuwa yeye alikuwa mwanajeshi kwa muda
mrefu, alijikuta ametopea kwenye madawa hayo lakini tiba pekee
iliyomfanya ajinasue kwenye madawa hayo ni Sober House.
“Mimi nilikuwa mwanajeshi kwa takriban kama miaka 10 na kitu lakini
nilifukuzwa jeshi kutokana na matumizi ya madawa ya kulevya, nikaenda
kutibiwa Kigamboni, kwa sasa nipo freshi kabisa.
“Naomba Mwenyezi Mungu anisimamie nisiweze kurudia maana yeye ndiye
anayetusaidia kuweza kufikia malengo yetu, sisi tunapanga lakini yeye
ndiye anayetuwezesha,” alisema Msilo.
Kabla ya kufikishwa kituoni hapo, Ray C alipoanza kuripotiwa na magazeti
ya Global Publishers kwa mara ya kwanza kuhusu kutopea kwenye madawa ya
kulevya, wadau mbalimbali waliguswa na hali mbaya aliyokuwa nayo
kitendo ambacho kilimgusa rais mstaafu, Jakaya Kikwete aliyemuita ikulu
na kumsaidia.
Title :
MENEJA WA SOBA HOUSE AELEZA SABABU ZA KUSKITISHA RAY C
Description : SIKU chache baada ya kufikishwa katika kituo maaulum cha kusaidia waathirika wa dawa za kulevya Bagamoyo Sober House, meneja wa kituo hi...
Rating :
5