Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam wameanza kudhibiti vitendo vya mauaji
kwa kupitia wapangaji na wenye nyumba kulazimika kuingia mikataba
itakayoambatana na picha ya mpangaji.
Wamewataka wenye nyumba wanapotengeneza mikataba waweke picha za
wapangaji wao na nakala zipelekwe kwenye ofisi za Serikali za mitaa kwa
ajili ya usalama.
Hatua hiyo imekuja baada ya jeshi hilo kubaini kuwa kila linapokwenda
kuwakamata watuhumiwa wanakoishi linakosa taarifa kamili kutoka kwa
wenye nyumba wao.
Kamanda wa Kanda hiyo, Simon Sirro alisema jana kuwa utafiti unaonyesha
wanapowafuatilia watuhumiwa, wengi wao huwa wamechukua chumba kimoja
ambacho hukaa miezi miwili hadi mitatu na baadaye wanahamia kwenye
nyumba nyingine.
Title :
POLISI DAR WABUNI MBINU MPYA ZA KUWANASA WATUHUMIWA WA MAUWAJI.......(SOMA ZAIDI)
Description : Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam wameanza kudhibiti vitendo vya mauaji kwa kupitia wapangaji na wenye nyumba kulazimika kuingia mikataba ...
Rating :
5