Leo July 19, 2019 Baada ya kutoa matamshi yaliyozua utata nchini Tanzania, Mbunge wa jimbo la Starehe nchini Kenya Charles Kanyi maarufu Jaguar ametua nchini Tanzania .
Kupitia akaunti ya Instagram Mbunge huyo alitupia picha ikionyesha ‘location’ kuwa yuko Dodoma na jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa BBC Swahili alisema kuwa amekuja Bongo kwa siku nne kuijulia hali familia yake mbali na kuwatembelea marafiki zake.
”Mimi naipenda Tanzania kwa sababu ni nchi nzuri na kama unavyojua nina kijana huku. Nawaambia Watanzania kwamba nawapenda sana na ndio sababu nimetembea hapa pia kama mtalii ili kuipatia kipato nchi hii”, Jaguar
Title :
Jaguar atua Tanzania kuiona famila yake
Description : Leo July 19, 2019 Baada ya kutoa matamshi yaliyozua utata nchini Tanzania, Mbunge wa jimbo la Starehe nchini Kenya Charles Kanyi maarufu ...
Rating :
5