Barcelona inataka kumsajili tena Neymar kutoka PSG, (Sport, via Express)
Kiungo wa Fulham Jean Michael Seri anajiandaa kujiunga na Galatasaray ya Uturuki kwa mkopo. (Mail)
Kocha wa Chelsea Frank Lampard ataamua kuhusu mchezaji Willian kama atapata mkataba mpya katika klabu hiyo. winga huyo, 30, amebakisha mwaka mmoja na Barcelona inamtaka mchezaji huyo kwa kitita cha pauni milioni 30. (Express)
Kocha mkuu wa Newcastle United Steve Bruce anaweza kutumia zaidi ya pauni milioni 90 katika dirisha la usajili. (Sky Sports)
Bruce 'alikuwa chaguo la 11' kwa ajili ya kazi hiyo ndani ya Newcastle. (Daily Mail)
Mshambuliaji wa zamani wa Newcastle Alan Shearer amesema alimwambia Bruce kutochukua kazi ya ukocha kwenye klabu . (Sun)
Hoffenheim wamethibitisha kuwa mshambuliaji Joelinton, 22, yuko kwenye ''mazungumzo ya kina'' na klabu hiyo na Newcastle United wana matumaini ya kuvunja rekodi kumnasa mchezaji huyo mwenye asili ya Brazil. (Chronicle Live)
Kocha wa Leicester Brendan Rodgers ameitahadharisha Mnchester kuwa kuna muda wa ukomo ikiwa wanataka kumsajili Harry Maguire, 26, (Star)
Kocha wa Leicester Brendan Rodgers amesifu utaalamu wa Harry Maguire, 26, na kukubali kuwa alikuwa ''ametulia'' kuhusu nia ya Manchester United kumnasa mlinzi huyo wa kati .(Independent)
Manchester United iko kwenye kinyang'anyiro cha kuwania saini ya kiungo wa Roma Nicolo Zaniolo. (Mirror)
Mshambuliaji Romelu Lukaku, 26, ana mpango wa kuondoka Manchester United na kuhamia Inter Milan. (Times - subscription required)
Unai Emery amesisitiza kuwa Arsenal wanafanya kazi kupata wachezaji ''watatu au wanne kabla ya kuanza msimu mpya. (Independent)
Kiungo Granit Xhaka yuko kwenye nafasi ya kuwa nahodha wa Arsenal akichukua nafasi ya Koscielny. (Telegraph)
Wadau wa klabu ya Juventus wamempa wakala wa Matthijs de Ligt mapokezi makubwa wakati alipoambatana na mchezaji huyo, mwenye miaka 19 kwa ajili ya vipimo siku ya Jumatano. (Metro)
Mchakato wa Arsenal kumpata mlinzi wa kikosi cha Celtic, raia wa Scotland Kieran Tierney huenda ukapata upinzani kumnasa mchezaji huyo. (Scotsman)
Arsenal imepewa angalizo kuwa haitaweza kufikia dau la Crystal Palace kwa ajili ya mshambuliaji Wilfred Zaha. (Mirror)
Pep Guardiola amefungua milango kwa Leroy Sane, 23, kuondoka Manchester City kwa kumwambia winga huyo anaweza kufanya hivyo kama hana furaha. (Mirror)
Burnley wana nia ya kumuuza golikipa wa kimataifa Tom Heaton wa England, kwa pauni milioni 12. (Birmingham Mail)
Ashley Cole amesababisha minong'ono kuwa yuko mbioni kuingia kwenye jopo la makocha wa Chelsea, baada ya kuweka picha yake akiwa uwanja wa ndege akielekea Japan. (Mirror)
Title :
Tetesi za usajili Ulaya Ijumaa 19.07.2019: Koscielny,Maguire,Neymar,Lampard
Description : Barcelona inataka kumsajili tena Neymar kutoka PSG, (Sport, via Express) Kiungo wa Fulham Jean Michael Seri anajiandaa kujiunga na Gala...
Rating :
5