Usafiri wa Mabasi Yaendayo Haraka maarufu kama mabasi ya Mwendokasi umekuwa tegemeo kuu kwa wasafiri Dar es Salaam lakini kwa siku mbili, huduma hiyo imekumbwa na vurugu.
Tatizo hilo lilizidi leo ambapo mabasi yaliadimika sana na yaliyopatikana abiria walilazimika kung'ang'ania nafasi ndani.
Baadhi walitumia madirisha badala la milango, mradi tu wajipate ndani ya mabasi hayo.
Je, chanzo ni nini?
Mkuu wa mawasiliano wa kampuni ya Usafiri Dar es Salaam Rapid Transit (UDA-RT), ililopewa wajibu wa kuendesha huduma hiyo, ametoa taarifa inayoashiria kuwa mgomo wa madereva ndicho chanzo kikuu cha kuvurugika kwa usafiri.
Taarifa ya Bw Deus Bugaywa iliyotolewa leo inaeleza kuwa kwa kawaida shughuli ya kutoa mabasi kutoka kwenye karakata kwenda kuhudumu barabarani hufanyika kwendo wa saa kumi kasorobo alfajiri.
Huduma hutakiwa kuanza saa kumi unusu na hivyo huwa kuna muda wa kutosha kwa madereva kuandaa magari tayari kwa safari.
Karakana ya mabasi hayo inapatikana eneo la Jangwani.
Leo, shughuli ilianza lakini badala ya kuendelea kama kawaida dereva mmoja alichukua basi na kuliegesha eneo la ndani la lango kuu la kutokea upande wa mbele na hivyo akawa ameziba njia. Mabasi mengine hayangeweza kutoka.
Basi lililotumiwa kuziba lango lilikuwa na urefu wa mita 18.
Kulikuwa na ndereva mwingine ambaye aliziba lango la nyuma kwa kutumia basi kama hilo.
Kutoroka na funguo
Baada ya kuziba milango mikuu, madereva hao wanadaiwa kuondoa funguo kutoka kwenye eneo la kuwashia magari na kukimbia hadi nje ya uzio na kutokomea.
Hii iliifanya vigumu kuyaondoa mabasi yaliyokuwa yameziba milango hiyo na ilihitaji mafundi kuitwa.
Taarifa ya Bw Bugaywa inasema walinzi walijaribu kuwafuata madereva hao wawili bila mafanikio.
Baadaye mafundi walifanikiwa kuyaondoa magari, lakini madhara yalikuwa tayari yametokea.
"Kazi hiyo ilifanikiwa lakini tayari ratiba ilikuwa imevurugika sana na kusababisha usumbufu mkubwa kwa abiria.
"Tunaamini kitendo hicho kilifanywa makusudi kwa lengo la kuhujumu mradi na ndio maana uchunguzi wa kina kwa kushirikiana na vyombo vya dola unafanyika ili kuwabaini tote waliohusika na njama hizo.
Tunaomba radhi abiria wetu kwa usumbufu uliojitokeza kutokana na kuchelewa kuanza huduma."
Mishahara ya madereva
Bw Bugaywa amekiri kamba kumekuwa na mzozo kuhusu mishahara ya madereva na wahudumu wa mabasi hayo.
Amesema mishahara ya wafanyakazi ya Septemba ilianza kulipwa Jumatatu, siku ambayo pia ilikumbwa na vurugu.
"Hatuoni saabu ya kuunganisha tukio hili na mishahara," amesema Bw Bugaywa.
Watanzania wamekuwa wakilalamika kwenye mitandao ya kijamii:
Athanas Pius ameandika: "Huu sio usafiri wa mwendokasi tena, sasa hivi ni mwendokusubiri ðŸ˜ðŸ˜. Watu mnajazana kituoni zaidi ya masaa mawili na hakuna gari. "
Title :
Sababu ya vurugu kukumba magari ya mwendo kasi Tanzania
Description : Image caption Mabasi ya mwendo wa kasi TZ Usafiri wa Mabasi Yaendayo Haraka maarufu kama mabasi ya Mwendokasi umekuwa tegemeo kuu kwa was...
Rating :
5