Moja ya sifa ya kuendelea kusalia kwenye nafasi ya ukocha ndani ya Real Madrid ni kutopoteza mechi ya mwisho kabla kuwaruhusu wachezaji kujiunga na timu zao za taifa hasa unapokuwa kwenye mwenendo mbaya wa ligi, kitu ambacho meneja Julen Lopetegui ameshindwa.
Kocha wa Real Madrid, Julen Lopetegui
Lopetegui amevunja sheria hiyo wikiendi hii baada ya kukubali kikosi chake cha Madrid kupoteza mbele ya Alaves na hivyo kuyafanya maisha yake ndani ya timu hiyo kuwa rahani.
Mourinho na rais wa Madrid, Florentino Perez
Mpaka sasa meneja huyo ameshapoteza michezo minne mfululizo pasipo kushinda hivyo wachambuzi wa maswala ya soka wanaamini anamuda mchache mno usiozidi hata mwezi mmoja kuendelea kuwa kwenye timu hiyo.
Gazeti maarufu la michezo nchini Hispania la ‘Diario AS‘ kwenye kurasa zake za mbele limeandika kuwa kocha huyo kama atachukua muda mrefu Real basi ni mpaka mechi ya ‘El Clasico’ mwishoni mwa mwezi wakati.
Majina ya makocha wanaotajwa kuchukua nafasi yake baada ya kutimuliwa ni, Jose Mourinho, Santiago Solari anaeifundisha Real Madrid B (Real Madrid Castilla) na Antonio Conte hii ikiwa ni kabla ya Christmas au mwishoni mwa msimu.
Inafahamika kuwa rais wa klabu ya Madrid, Florentino Perez ni rafiki na shabiki mkubwa wa Mourinho lakini nimapema mno kumuita Mreno huyo na hivyo anasikilizia nguvu ya mashabiki.
Conte ni moja kati ya makocha wachache waliyokuwa kwenye listi hiyo, Solari ambaye amewahi kuwa mchezaji wa Madrid na kocha wa kikosi B anapigiwa upatu kuifundisha timu hiyo.
Ikiwa baadhi ya wachezaji wakijiunga na timu zao za taifa Perez na Lopetegui wanazidi kuwa kwenye wakati mgumu baada ya kushindwa kufanya usajili mkubwa ambao utaziba pengo linaloonekana kwa sasa baada ya kumuuza nyota wake Ronaldo kwa euro milioni 100.
Wachezaji kama Isco, Dani Carvajal na Marcelo wakiwa wanasumbuliwa na majeraha mara kwa mara wakati Gareth Bale na Karim Benzema wakiwa wapo chini ya kiwango nakufanya kocha Lopetegui mwenye umri wa miaka 52 kuwa kwenye nafasi mbaya zaidi katika kazi yake.
Title :
Mourinho anukia kutua Real Madrid, hatma ya Julen Lopetegui kujulikana mwisho wa mwezi huu
Description : Moja ya sifa ya kuendelea kusalia kwenye nafasi ya ukocha ndani ya Real Madrid ni kutopoteza mechi ya mwisho kabla kuwaruhusu wachezaji kuji...
Rating :
5