Leo October 8, 2018 Ninayo stori kumhusu Dereva aliyemruhusu Nyani kuendesha basi lililokuwa limebeba abiria nchini India hatimaye amefukuzwa kazi baada ya video ya tukio hilo kusambaa katika mitandao ya kijamii na kuwafikikia serikali na wamiliki wa basi hilo.
Katika video iliyokuwa ikisambaa katika mitandao ya kijamii ilimuonesha Prakash mwenye umri wa miaka 36, akimuachia nyani kuketi juu ya uskani wa basi hilo na kuendesha huku dereva huyo akionekana kufurahishwa na kitendo hiko.
Msemaji wa kampuni ya usafiri wa barabara nchini India Kartanaka amesema kitendo hicho kimesababisha wamiliki na serikali kumfukuza kazi dereva wa basi hilo ambalo lilikuwa na abiria takribani 30, kitendo ambacho kina kinzana na kanuni na taratibu za usafiri nchini humo.
Title :
Kilichomkuta Dereva aliemuachia nyani kuendesha gari
Description : Leo October 8, 2018 Ninayo stori kumhusu Dereva aliyemruhusu Nyani kuendesha basi lililokuwa limebeba abiria nchini India hatimaye amefu...
Rating :
5