Nyota wa klabu ya Liverpool na Misri Mo Salah ametishia kujiondoa katika timu ya taifa lake kufuatia habari kwamba amekuwa hana raha na kile kilichotokea nchini Chechnya ambapo timu hiyo imepiga kambi wakati wa kombe la dunia la Urusi 2018.
Msimu uliopita Salah alipata jeraha katika mechi dhidi ya Real Madrid na kukosa mechi ya kwanza ya Misri dhidi ya Uruguay licha ya kucheza na kufunga dhidi ya Urusi ambapo Misri ilipoteza 3-1.
Na huku akiendelea kutaabika na jeraha, picha ya Salah akitembea na rais wa Chechnya Ramzan Kadyrov ilizungumziwa sana katika kombe la Dunia.
Wakati huohuo kadyrov alimpatia Salah uraia wa heshima wa jamuhuri ya Chechnya.
''Mohammed Salah ni raia wa heshima wa jamhuri ya Chechnya! Huo ni ukweli!'', Kiongozi huyo wa Chechnya aliandika katika chapisho la mitandao ya kijamii.
''Nilimpatia Mo Salah nakala ya agizo hilo na pini yake katika sherehe ya chakula cha jioni kwa heshima ya timu ya taifa la Misri''.
Kituo cha habari cha serikali ya Urusi RT kilionyesha Salah akitabasamu huku kadyrov akitoa hotuba yake na kuweka beji katika tisheti ya mchezaji huyo wa Misri.
Hatahivyo shirikisho la soka nchini Misri FA limesema kuwa madai ya kwamba Salah anataka kujiondoa katika timu hiyo ya taifa sio ya kweli.
''Mo bado yuko nasi na ana furaha kuwa nasi katika kambi yetu. Anakula na kucheka na wachezaji wenzake''. Anafanaya mazoezi vizuri na hiyo inamaanisha kwamba hana wasiwasi''.
Kadyrov amelaumiwa kwa kumtumia mchezaji huyo kuendeleza propanganda zake za kisiasa.
Misri imepiga kambi Chechnya wakati wa kombe la Dunia , na siku ya Jumamosi ajenti wa Salah alituma ujumbe katika mtandao wa Twitter akidai kwamba Salah amekasirika.
Utawala wa Kadyrov umekuwa ukilaumiwa kwa ukandamizaji wa haki za kibinaadamu, madai aliyopinga wiki hii katika mahojiano na BBC.
Salah alikwaruzana na shirikisho la soka nchini Misri kuhusu haki za picha zake.
Alikasirika baada ya picha yake kutumika kukuza mafadhili rasmi WE wakati alipokuwa na mkataba wa ufadhili na mahasimu wake Vidafone.
Alituma ujumbe wa twitter kwa lugha ya kiarabu akisema: ''Pole lakini haya ni matusi makubwa''.
Salah anahisi kwamba ametumika vibaya kwa kile kilichofanyika Chechnya.
Mchezaji huyo wa Liverpool hapendelei kujishirikisha katika mazungumzo mbali na kandanda ama kutumika kisiasa.
Title :
Mohamed Salah akasirika na kutishia kujiondoa katika kikosi cha Misri
Description : Nyota wa klabu ya Liverpool na Misri Mo Salah ametishia kujiondoa katika timu ya taifa lake kufuatia habari kwamba amekuwa hana raha na k...
Rating :
5