Leo June 14, 2018 Naibu waziri wa Kilimo, Dk Mary Mwanjelwa amempongeza Mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe (ACT –Wazalendo) kwa kuuliza swali zuri na kumuomba amletee nakala ya mkakati ili waifuatile
Awali mbunge huyo alisema kuwa February mwaka jana kamati ya maendeleo ya Mkoa RCC ilipitisha mkakati wa kuendeleza zao la mchikichi wizarani lakini hadi leo bado hawajajibiwa.
Alisema kutojibu huko kunaweza kuthibitisha kwamba serikali imeshikwa na wafanyabiashara wa mafuta hayo ya kula wanaoagiza kutoka nje, alitaka kueleza sababu za kukaa kimya.
Akijbu , Naibu waziri Mwanjelwa alisema kuwa mbunge huyo ameuliza swali zuri na kumuomba kumpatia nakala ya mkakati huo ili wizara ifuatilie na kuifanyia kazi.
Kuhusu kusuasua kwa vituo vingi vya maendeleo ya kilimo , alisema kuwa inatokana na upatikanaji wa fedha. Aidha aliviomba vyuo vya utafiti wa kilimo kujiongeza na kutokutegemea fedha za serikali. Alisema vituo hivyo vinaweza kuandika maandiko mbali mbali kwa wafadhili kwa ajili ya kupata fedha za utafiti na maendeleo.
Title :
Barua aliyotakiwa kuiwasilisha Zitto Kabwe kwa Naibu Waziri wa Kilimo Mwanjelwa
Description : Leo June 14, 2018 Naibu waziri wa Kilimo, Dk Mary Mwanjelwa amempongeza Mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe (ACT –Wazalendo) kwa kuuliz...
Rating :
5