Staa maarufu kutokea Marekani Akon mwenye asili ya Senegal amezidi kuwashangaza mashabiki wake baada ya kutangaza rasmi kuja na mfumo wa hela ya kidigitali wakati alipokuwa katika tamasha la Cannes Lions lililofanyika France siku ya Jumatatu June 18,2018 na kusema kuwa mfumo huo utaisaidia Afrika kiuchumi.
Ameeleza chini ya kuwa katika mazingira ya mfumo wa hela ya kidijitali inayoitwa“Akoin” mtu ataweza kununua , kuhifadhi na kutumia moja kwa moja kutoka kwenye simu ya mkononi na anataka mfumo huo uanze sasa mpaka mwezi December.
Pia Akon amesema kuwa amekuja na mradi huo na anataka wataalamu wa teknolojia wakae chini walishughulikie suala hilo na kusema kuwa mfumo huo utawaruhusu watu kuutumia kwa njia ambayo wanaweza kujiendeleza na kutoruhusu serikali kufanya mambo yanayowakwamisha kimaendeleo.
Katika tamasha hilo staa Akon ameeleza kuwa anampango pia wa kuwa na mji wake utakaoitwa “Wakanda” ambapo mji huo utakua na mazingira na mandhari ya filamu ya “Black Panther” ikiwa mji huo utajengwa katika ardhi ya heka 2000 aliyokabidhiwa na Rais wa Senegal.
Title :
AKON na mpango wa kutengeneza “Fedha” yake na mji wa ‘Wakanda’
Description : Staa maarufu kutokea Marekani Akon mwenye asili ya Senegal amezidi kuwashangaza mashabiki wake baada ya kutangaza rasmi kuja na mfu...
Rating :
5