Baada ya kutokuwa na maelewano mazuri kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda na Mkurugenzi wa vipindi wa Media Clouds Group. Hatimae leo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amewataka kumaliza tofauti hizo huku akiwataka waongozane wakishikana mikono.
Rais Magufuli amewakutanisha viongozi hao mkoani Tanga ambapo yupo na Mgeni wake Yoweri Museveni Rais wa Uganda katika uzinduzi wa Mmradi Bomba la Mafuta kutoka Hoima – Uganda hadi bandari ya Tanga.
“Nakupongeza sana Ruge sijui uko hapa .Ruge yupo embu njoo hapa bwana yuko wapi Ruge leo hayupo? Ruge nakupongeza sana kwa kazi nzuri kwenye kikundi hiki, Makonda njoo mbele ninawaleta vijana wote nawapenda nawaonataka wapendane shikaneni mikono hapa nataka mambo yenu nyinyi wawili yaishe nataka mfanye kazi kwaaajili ya Tanzania,Nakupongeza Ruge kwa kazi nzuri na Mungu awabariki sana asanteni sana nendeni mkishikana mikono,” amesema Rais Magufuli.
Title :
Ruge na RC Makonda uso kwa uso
Description : Baada ya kutokuwa na maelewano mazuri kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda na Mkurugenzi wa vipindi wa Media Clouds Group. Hatim...
Rating :
5