Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amewahakikishia watu wa Muheza kuwa hata badilika huku akisisitiza kuwa atalala mbele na mafisadi na kuyatumbua kikamilifu.
Ameyasema hayo leo wakati akiwa katika ziara ya mjini Tanga wakati akihutubia wananchi wa Muheza.
“Wanamuheza na Watanzania kwa ujumla waliamua kwamba Rais atakuwa Magufuli na mimi baada ya kuteuliwa kuwa Rais nataka niwahakikishie sita badilika nitalala mbele na haya mafisadi nitayatumbua mpaka yatumbuke kikamilifu, muheza oyeee sitaangalia sura zao, sitaangalia utajiri wao nitakachoangalia ni maslahi ya Watanzania maskini ambao wameteseka kwa muda mrefu,” amesema Rais Magufuli.
Aidha Rais Magufuli amesema Tanzania ilishakuwa imekuwa kawaida wajane wamadhulumika hawaangaliwi huku wajane wamekuwa wakinyanga’nywa mashamba yao amesema kuwa haiwezi kuiacha nchi ya Tanzania katika hali hiyo.
Hata hivyo Rais Magufuli yupo Tanga ambapo Agosti 5 atakutana na Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi la Mradi wa bomba la kusafirisha mafuta Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga.
Title :
Nitalala mbele na mafisadi – Rais Magufuli
Description : Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amewahakikishia watu wa Muheza kuwa hata badilika huku akisisitiza kuwa at...
Rating :
5