Siku chache baada ya Serikali kupitia msemaji wake mkuu (Idara ya habari Maelezo) Dkt. Hassan Abbasi kujibu hoja zilizotolewa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuhusu hali ya kiuchumi kwa sasa kwa kile walichodai ni mbaya. Leo Waziri kivuli wa fedha na uchumi wa kambi rasmi ya Upinzani bungeni, Halima Mdee ameijibu Serikali kwa kusema majibu yaliyotoa kuhusu hali ya uchumi kwa sasa hayana ukweli.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Makao makuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) yaliyopo jijini Dar es salaam ambapo amelinganisha aliyoyasema Msemaji wa serikali.
Msemaji: Kwa kwa mujibu wa farihisi ya uwekeza Afrika iliyotolewa na QUANTUM GLOBAL RESEARCH LAB ya Uingereza ya mwaka huu Tanzania ni ya kwanza katika EAC kwa kuvutia wawekezaji.
Mdee: Kweli hili serekali imezidi kusema uongo na au kupotosha umma kwa makusudi, kwa mujibu wa taarifa hiyo ya mwezi Mei, 2017 ukurasa wa 15 & 16 nchi za Afrika zimeorodheshwa na Tanzania sio ya kwanza kwa upande wa Afrika Mashariki bali ni ya pili baaday ya Kenya, Tanzania ni ya tano wakati Kenya ni ya pili na Uganda ni ya Sita katika uwekezaji.
Sababu kubwa iliyoifanya Tanzania na Uganda kuwa katika nafasi za juu zilitokana na ugunduzi wa mafuta na gasi uliogundulika katika nchi hizi.
Msemaji: Kwamba bajeti wizara ya Afya imeongezeka na hasa kwenye dawa kutoka bilioni 30 mwaka 2015/16 hadi bilioni 251 kwa mwaka 2016/17
Mdee: Kwa mujibu wa taarifa za wizara ya afya zilizowasilishwa kwenye kamati ya bunge (randama) mpaka mwezi Machi 2017, wizara ilikuwa imepokea sh. 314.673 bilioni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na miradi ya maendeleo kiasi ambacho ni sawa asilimia 40 tu ya fedha zote zilikuwa zimetengwa na bunge.
Kwa hiyo sio kiwango kilichopitishwa kwenye bajeti bali ni kiasi gani halisi kilifikishwa wizara?, je kuna uhakika gani kuwa zilizotengwa sasa zitapelekwa?
Kwamba mikopo elimu ya juu mwaka 2016/17 zilitengwa sh. bilioni 483 na bajeti ya sasa 2017/2018 zimetengwa sh. bilioni 427.
Hapa napa serikali pongezi kwa ujasiri wa kukukiri kuwa mikopo elimu ya juu imepungua wakati idadi ya waafunzi wahitaji imeongezeka. Serikali inaposhindwa kugharimia elimu ya vijana wake na wakati huo inasemakana uchumi umeimarika haiwezi kueleweka, maana kipaumbele cha nchi maskini ni kuwekeza katika elimu ili ipate wataalamu wa kutosha kuwakwamua katika umasikini huo. Tusitengemee rasimali za asili tu bali lazima sasa tuwekeze kwenye elimu ili tuweze kuuza huduma.
Title :
Halima Mdee kaja na hili kwa serikali kuhusu hali ya uchumi
Description : Siku chache baada ya Serikali kupitia msemaji wake mkuu (Idara ya habari Maelezo) Dkt. Hassan Abbasi kujibu hoja zilizotolewa na Chama cha ...
Rating :
5