Ni mwezi mmoja umepita baada ya Kampuni ya Apple kutangaza kuwa watajikita katika utengenezaji wa magari yanayojiendesha yenyewe, tayari mshindani wake kibiashara kampuni ya Samsung nao wamepata kibali cha kutengeneza magari hayo.
Samsung wamepata kibali cha kutengeneza magari hayo kutoka kwa Serikali ya Korea Kusini ambako ndiyo makao makuu ya kampuni hiyo yaliko, huku wakijinadi kuwa wamefikia uamuzi wa kutengeneza magari hayo kuendana na teknolojia.
Taarifa kutoka mtandao wa
Thenextweb zimeeleza kuwa Samsung wataanza kwanza majaribio yao na Kampuni ya magari ya Hyundai na baadae kutengeneza magari yao wenyewe.
“Lengo kubwa la Kampuni yetu ni kuhakikisha dunia inakuwa salama zaidi sio tu kwa mazingira bali hata viumbe hai ndiyo maana kila kukicha tunajitahidi kuleta vitu vipya,Teknolojia hii (Magari yanayojiendesha yenyewe) itasaidia kupunguza msongamano,Kupunguza ajali na kulinda mazingira“Alisema Afisa mipango wa Kampuni ya Samsung Bw. Young Sohn.
Mwishoni mwa mwaka jana Samsung walinunua kampuni ya HARMAN inayojihusisha na utengenezaji wa vifaa vya ndani vya magari kwa Dola Bilioni 8 za kimarekani hivyo huenda ilikuwa ni njia ya kujiwekea urahisi kwa kampuni hiyo kuingia kwenye teknolojia ya magari yanayojiendesha hivyo tutarajie kuona magari ya kampuni hiyo yenye nguvu zaidi duniani.
Kwa sasa bei ya magari hayo haijatajwa, kutokana na sababu za kibiashara .
Kampuni ya Samsung itaungana na makampuni mengine makubwa Duniani kama Tesla, Apple,Google na mengine kibao kwenye ushindani wa soko la magari yanayojiendesha yenyewe.
Na Albert Luhogola
Title :
Soko la magari yanayojiendesha yenyewe lazidi kukua; Samsung nayo ndani
Description : Ni mwezi mmoja umepita baada ya Kampuni ya Apple kutangaza kuwa watajikita katika utengenezaji wa magari yanayojiendesha yenyewe, tayari m...
Rating :
5