Staa wa kibao, Muziki, Shariff Thabit alamaarufu Darassa, kwasasa hashikiki kwa jinsi alivyopanda chati kwa ghafla kwenye muziki wa kizazi kipya Africa. Darassa ambaye kwasasa ameachia kibao kingine kikali pamoja na video yake, amemwaga petroli kwenye moto uwakao. Niajabu kuwa Darassa bila ya kutumia kiki, ameweza kukubalika kirahisi kinyume kabisa na wasanii wengine wakali Africa Mashariki. Kupitia makala haya, nitakupa nafasi ya kubaini mwenyewe ukweli huu wa mambo ambao haufichiki ja kinga cha moto kilicho fichwa chini ya majani yaliyo kauka.
Takribani wiki mbili zilizopita, Darassa akiandamana na Ben Paul na AY ambaye Darassa amenukuliwa kusema yeye ndiye anayempa na kumuonesha njia zakupitia ilikuyafikia malengo yake kimuziki, waliitembelea nchi ya Kenya kwa ajili ya kupiga show mjini Nairobi na pia kufanya media tour yake ya kwanza nchini humu. Na kwakweli kupitia kanda za video ambazo ninakukonyezea hapa chini utakubaliana nami kuwa Darassa yuko katika level nyingine kabisa tofauti na wasanii wengine wa Tanzania na Africa Mashariki kwa jumla. Kati ya vyombo vya habari alivyowahi kuvitembelea, vilikuwemo viwili vikubwa si Kenya pekee bali humu barani Africa nikizungumuzia Citizen TV na NTV.
kipindi maarufu cha Burudani #TheTrend, kinacho rushwa hewani kila siku ya Ijumaa na kinacho endeshwa na mtangazji maarufu Larry Madowa. Darassa pia alifunguka na kwa mara ya kwanza wakenya ama mashabiki wake walipata fursa yakujua kuwa Msanii mkali na staa wa Zigo Ambweni Yesaya aka AY pia ni mmoja ya wadau wanao msaidia kuzikwea ngazi za juu kimuziki
Title :
Mapokezi ya Darassa Kenya Ni Moto Wa Kuotea Mbali
Description : Staa wa kibao, Muziki, Shariff Thabit alamaarufu Darassa, kwasasa hashikiki kwa jinsi alivyopanda chati kwa ghafla kwenye muziki wa kiz...
Rating :
5