Okinoshima – Japan ndicho kisiwa kisichowaruhusu wanawake bali wanaume pekee kuzuru kisiwa hicho.
Jopo la ushauri limependekeza Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), itambue kisiwa hicho kama turathi ya ulimwengu. Uamuzi unatarajiwa kufanywa katika mkutano wa Unesco mwezi Julai mwaka huu.
Kisiwa cha Okinoshima, hutumika kufanya matambiko kwa ajili ya usalama wa meli na pia wakazi wa Japan hutumia kisiwa hicho kuwasiliana na wakazi wa rasi ya Korea na China kati ya karne ya nne na tisa.
Katika kisiwa kuna miiko kama vile wanawake kutofika hapo pamoja na wageni wa kiume kutakiwa kuvua nguo zote kabla ya kufanya tambiko la kujitakasa. Aidha, hawatakiwi kufichua chochote kuhusu walichoshuhudia wakiwa kwenye ksiwa hicho.
“Haya ni baadhi ya mambo ambayo itabidi yazingatiwe iwapo kisiwa kitaorodheshwa kuwa turathi,” anasema Asahi Shimbun, na kueleza kuwa huenda kisiwa hicho kikawa maarufu sana kwa utalii.
Hata hivyo, bado hakuna uwezekano kwamba marufuku dhidi ya wanawake kufika katika kisiwa hicho kitaondolewa.
By Albert Luhogola
Title :
Fahamu : Kisiwa ambacho ni marufuku kwa wanawake kufika
Description : Okinoshima – Japan ndicho kisiwa kisichowaruhusu wanawake bali wanaume pekee kuzuru kisiwa hicho. Jopo la ushauri limependekeza Sh...
Rating :
5