Serikali imetoa tathmini ya hali ya mfumuko wa bei nchini kupitia Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS). Takwimu zimeonyesha mfumuko wa bei wa Taifa kwa mwezi Aprili umebaki kuwa ni asilimia 6.4% kama ilivyokuwa mwaka uliopita.
Mkurugenzi wa Sensa za watu na Takwimu Ofisi ya Taifa ya Takwimu,(NBS), Ephraim Kwesigabo, akizungumza na waandishi wa habari.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Sensa za watu na takwimu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu,(NBS) Ephraim Kwesigabo, amesema hii inamaanisha kuwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioisha March 2017 imekuwa sawa na kasi ya upandaji ilivyokuwa mwaka ulioisha.
Kwesigabo, alisema fahirisi za bei zimeongezeka hadi 109.4 mwezi April 2017 kutoka mwezi April 2016.
“Mfumuko wa bei kwa kipimo cha mwaka umebaki kuwa asilimia 6.4 kama ilivyokuwa mwezi marchi 2017 kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioisha mwezi Aprili imekuwa sawa na mwezi Marchi 2017,”alisema Kwesigabo .
Pia alisema mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi Aprili 2017 umeongezeka hadi 11.8 kutoka asilimia 11.0 ilivyokuwa mwezi Marchi 2017.
Aidha mfumuko wa bei kwa kipimo cha mwaka kwa bidhaa za vyakula nyumbani na migahawani kwa mwezi Aprili 2017 umeongezeka hadi asilimia 12.0 kutoka asilimia 11.7 mwezi Marchi 2017.
Hata hivyo badiliko la fahirisi za bei kwa bidhaa sisizo za vyakula umepungua kidogo hadi asilimia 3.4 mwezi Aprili kutoka asilimia 3.6 mwezi Marchi 2017.
Akizungumzia kuhusu ukuaji wa dhamani ya shilingi, Kwesigabo amesema uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma umefikia shilingi 91 na senti 71, mwezi Aprili 2017 ikilinganisha na shilingi 92 na senti 21 ilivyokuwa mwezi Marchi 2017.
Title :
NBS watoa takwimu za mfumuko wa bei nchini
Description : Serikali imetoa tathmini ya hali ya mfumuko wa bei nchini kupitia Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS). Takwimu zimeonyesha mfumuko wa bei wa Ta...
Rating :
5