Rais Barack Obama ameiomba jumuiya ya wamarekani wenye asili ya Afrika kusaidia kumzuia Donald Trump, akidai kuwa atachukulia kama tusi kwa heshima yake ikiwa wapiga kura weusi wasipompigia kura Hillary Clinton.
Akiongea kwa mara mwisho kwenye mkutano wa jumuiya ya watu weusi, Obama aliwaasa watu wengi kujitokeza kupiga kura. Hotuba ya Obama inakuja miezi miwili kabla ya uchaguzi.
Obama pia alielezea kwa mafumbo suala ya Trump hatimaye kukubali kuwa alizaliwa Marekani. Kwa muda mrefu Trump alikuwa anabisha kuwa Obama hakuzaliwa Marekani na alitaka aoneshwe cheti chake cha kuzaliwa ili aamini.
Obama alimuelezea Trump kama mtu ambaye amekuwa akipingana na haki za raia na usawa na kwamba ni mtu asiye na heshima kwa wafanyakazi kwa miaka yote.
Title :
UCHAGUZI MAREKANI,OBAMA ASEMA HAYA.
Description : Rais Barack Obama ameiomba jumuiya ya wamarekani wenye asili ya Afrika kusaidia kumzuia Donald Trump, akidai kuwa atachukulia kama tusi kwa...
Rating :
5