Rapper Nelly yupo kwenye wakati mgumu kutokana na deni alilonalo la $2,412,283 kutokana na malimbikizo ya kodi.
Pia rapper huyo anadaiwa na idara ya mapato ya Missouri $149,511 za kodi kuanzia mwaka 2013.Mashabiki wake wameendelea na mkakati wa kumsaidia rapper huyo fedha kwa kusikiliza muziki wake mtandaoni kwa kasi ya ajabu.
Usikilizwaji wa muziki wa Nelly kwenye mtandao wa Spotify umeongezeka kwa asimilia 200. Si rahisi lakini kwakuwa mashabiki wanapaswa kusikiliza muziki wake mara 402,880,500 ili kufikisha kaisi cha $2.4m.
Wakati mashabiki wakifanya yao, sasa IRS imedaiwa kutaka kukata hela yao kupitia fedha anazopata kwenye ziara yake. Nelly ana show nne zinazokuja ambazo IRS imewasiliana na kampuni inayokata tiketi zake show zake ili kukata fedha hizo.
Title :
MASHABIKI WAJIPANGA KUMSSAIDIA RAPPER NELLY KULIPA DENI
Description : Rapper Nelly yupo kwenye wakati mgumu kutokana na deni alilonalo la $2,412,283 kutokana na malimbikizo ya kodi. Pia rapper huyo anada...
Rating :
5