Jeshi la Korea Kusini linasema Korea
Kaskazini imerusha makombora matatu ya masafa marefu baharini saa
chache baada ya Rais wa Korea Kusini Park Geun-hye kukutana na Rais wa
Uchina Xi Jinping pambizoni mwa mkutano mkuu wa nchi 20 zenye
zilizostawi zaidi kiuchumi duniani.
Makombora hayo yalirushwa kutoka eneo la Hwangju.
Bi
Park ametoa wito wa kuwepo kwa ushirikiano zaidi na Uchina, ambayo ni
mshirika wa Korea Kaskazini, kuhusu kile alichosema ni uchokozi wa mara
kwa mara wa Pyongyang ambayo imekuwa ikifanya majaribio ya mabomu ya
nyuklia na makombora.
Vyombo vya habari Uchina vimesema Xi
amesisitiza pingamizi zake dhidi ya kujengwa kwa mfumo wa Marekani wa
kujikinga dhidi ya makombora nchini Korea Kusini.
Amesema mpango huo huenda ukazidisha uhasama
Title :
KOREA ITARUSHA MAKOMBORA KWENYE MKUTANO WA G20 UKIENDELEA
Description : Jeshi la Korea Kusini linasema Korea Kaskazini imerusha makombora matatu ya masafa marefu baharini saa chache baada ya Rais wa Korea...
Rating :
5