Wanafunzi 10 wa Shule ya Sekondari Mnara iliyoko, Wilaya ya LINDI wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa ya SOKOINE mjini LINDI
Mkuu wa Mkoa wa LINDI, GODFREY ZAMBI
Wanafunzi 10 wa Shule ya Sekondari Mnara iliyoko, Wilaya ya
LINDI wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa ya SOKOINE mjini LINDI, baada
ya kuanguka kutoka katika lori wakati wakielekea NGONGO kwenye Maonesho
ya wakulima NaneNane.
Ajali hiyo imetokea katika Kijiji cha RUTAMBA barabara ya RONDO,
baada ya dereva wa lori hilo kukwepa korongo hali iliyosababisha gari
kulalia upande mmoja ambapo mabomba waliyokuwa wamejishikilia wanafunzi
hao yaling’oka na wanafunzi wote pamoja na walimu waliokuwa wamepakiwa
kuanguka chini.
Kwa mujibu wa mkuu wa Mkoa wa LINDI, GODFREY ZAMBI amesikitishwa na
ajali hiyo na hali ya majeruhi kuchukua muda mrefu bila kupata huduma.
Title :
WANAFUNZI 10 WALAZWA BAADA YA KUANGUKA KUTOKA KWENYE ROLI
Description : Wanafunzi 10 wa Shule ya Sekondari Mnara iliyoko, Wilaya ya LINDI wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa ya SOKOINE mjini LINDI Mkuu wa ...
Rating :
5