Kila siku
asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti
ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya
Twitter >>>@millardayo. Tayari nimezikusanya na waweza
kuzipitia hapa chini moja baada ya nyingine.
Moja ya story kubwa June 06 2016 kwenye gazeti la Jambo leo ni hii yenye kichwa cha habari ‘Hoja kukata mishahara ya wabunge yakwama’
Gazeti
hilo limeeleza kuwa mara baada ya kuanza kwa mgomo wa wabunge wa
upinzani May 30 2016, baadhi ya wabunge wamekuwa wakiomba miongozo
bungeni kutaka ufafanuzi endapo wabunge waliosusia vikao wanapaswa
kulipwa posho kamili sawa na wenzao wanaoendelea na vikao.
Gazeti
hilo limeripoti kuwa jana Naibu Spika Dk. Tulia Ackson alijibu miongozo
hiyo akibainisha kuwa wabunge hao wataendelea kulipwa posho zao kamili
kwani hakuna sheria zinazozuia malipo ya mishahara na posho za wabunge
hao.