Tarehe 20 mwezi februari mwaka 1969, walemavu saba wa macho waliweza kumaliza kupanda mlima Kilimanjaro uliopo Tanzania.
Mlima huo ambao ni mrefu zaidi Afrika kwa mita 5,750 (18,865ft) , kundi hilo walemavu waliokuwa wanasindikizwa na watu wanne wanaoona waliweza kutumia saa tisa kumaliza mita 914.4 ambayo ni sawa na futi 3,000.
Safari hiyo ya kupanda mlima, ambayo ilifadhiliwa na muasisi wa shirika la kujitolea la 'Charity sighter' lililenga kusaidia kupata picha ya ulemavu wa macho barani Afrika na kuonesha namna ambavyo walemavu wa macho wakipata mafunzo wana uwezo wa kutimiza malengo yao au kufanya chochote wanachokipenda.
Walemavu nane kati ya tisa waliweza kumaliza safari yao lakini mmoja wao alishindwa kuendelea.
"Siku ambayo tulianza kupanda mlima, wawili wetu waliugua njiani kutokana na mazingira waliokutana nayo," Geoffrey Salisbury kutoka jumuiya ya walemavu wa macho Sightsavers alisema.
"Jambo ambalo lilitusumbua lilikuwa ni kupigwa na mionzi ya jua moja kwa moja kwenye uso.
Tuliweza kukutana na theluji kwa mara ya kwanza". John Opio ambaye alikuwa anaumwa kichwa baada ya kupanda mlima Kilimanjaro.
Maumivu yalikuwa makali kwa John Kisaka kutoka Tanzania mpaka akaomba kuishia njiani.
Wapandaji wasioona walichaguliwa kutoka kwa washiririki mia moja waliokuwa wamejitolea kushiriki kutoka Kenya, Uganda na Tanzania.
Kabla ya kupanda mlima , walifanya mazoezi ya wiki mbili ambayo yalijumuisha namna ya kupanda mlima kwa kutumia kamba, kukaa kwenye kambi ya usiku na namna ya kutumia vifaa vya kupandia mlima.
Zoezi hilo la upandaji mlima liliandikwa katika kurasa za mbele katika magazeti yote barani Afrika ,wakilakiwa kama mashujaa.
Washindi wa mlima huo walizawadiwa viatu ambavyo vimehifadhiwa katika makumbusho ya taifa ya Uganda.
Title :
Walemavu wa macho waliopanda mlima Kilimanjaro
Description : Tarehe 20 mwezi februari mwaka 1969, walemavu saba wa macho waliweza kumaliza kupanda mlima Kilimanjaro uliopo Tanzania. Mlima huo ambao...
Rating :
5