Ndege ya mizigo imeanguka katika bahari ya Atlantiki karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa huko Abidjan nchini Ivory Cost huku watu wanne wakidaiwa kufariki na wengine sita wakitaarifiwa kuumia hii leo siku ya Jumamosi.
Taarifa zinasema kuwa watu 10 walikuwa ndani ya ndege hiyo iliyokuwa ikitokea Burkina Faso, Kamanda wa jeshi la zimamoto, Lt. Issa Sakho amezungumza kupitia chombo cha habari cha taifa kuwa wa Moldova wanne wamefariki nakuongeza kuwa Moldova wawili na wajumbe wanne wa Ufaransa wamejeruhiwa.
Kamanda, Sakho amesema walikuwemo watu 10 wakitokea nchi jirani na kuongeza kuwa ajali hiyo ya ndege haikusababisha uharibifu wowote chini ya ardhi wakati wa kuanguka kwake.
Msemaji wa majeshi ya Ufaransa aliyopo Ivory Coast amesema watu sita wamejeruhiwa kutoka katika ndege hiyo ya mizigo iliyoanguka.
Msemaji huyo amesema hana idadi kamili ya watu waliyo fariki ama abiria.
Kamanda Lt. Villain hakutaja jina lake kamili akifuatataratibu za Kifaransa, amesema kuwa ndege hiyo ilikuwa imebeba mizigo ya jeshi la Ufaransa na waliyoumia wamepelekwa katika kambi ya Port-Bouet iliyopo Abidjan kwa matibabu.
Title :
Ndege ya mizigo yaanguka baharini
Description : Ndege ya mizigo imeanguka katika bahari ya Atlantiki karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa huko Abidjan nchini Ivory Cost huku watu wanne w...
Rating :
5