Mwanamuziki maarufu amekamatwa kwa kucheza ''dabbing'' wakati wa tamasha kusini magharibi mwa Saudia.
Mwanamuziki maarufu amekamatwa kwa kucheza ''dabbing'' wakati wa tamasha kusini magharibi mwa Saudia.
Abdallah Al Shahani, mtangazaji wa runinga, muigizaji na raia wa Saudia alikuwa akionyesha miondoko hiyo ya densi ya dabbing ambayo inashirikisha mcheza densi kuingiza kichwa chake chini mkono katika tamasha la muziki katika mji wa Taif wikendi iliopita.
Dabbing imepigwa marufuku katika taifa hilo la kihafidhina ambapo utawala unaifananisha na utamaduni wa utumizi wa mihadarati.
Kanda ya video ya densi hiyo ya bwana Al Shahani ilikuwa maarufu katika mitandao ya kijamii na maelfu wametuma ujumbe katika mtandao wa Twitter kuhusu kisa hicho.
Inadaiwa kuwa dabbing inatoka katika muziki wa Hip- Hop katika jimbo la Atlanta, Georgia, Marekani, takriban miaka miwili iliopita lakini ikapata umaarufu baada ya watu maarufu , wanariadha na wanasiasa ikiwemo Hillary Clinton na Paul Ryan kuanza kuonyesha densi hiyo.
Title :
Mwanamuziki wa Saudia Akamatwa Kwa Kucheza Dab
Description : Mwanamuziki maarufu amekamatwa kwa kucheza ''dabbing'' wakati wa tamasha kusini magharibi mwa Saudia. Mwanamuziki maar...
Rating :
5