Halmashauri ya manispaa ya Kinondoni jijini Dar es salaam imetangaza kujenga kituo kipya cha kisasa cha Daladala katika eneo la Kawe maarufu eneo la Gereji ili kuondoa Adha kwa waendesha daladala , pamoja na wananchi wanaotumia barabara ya kawe kutokana na kutokuwapo kituo cha mabasi katika barabara hiyo.
Mstahiki Meya wa Kinondoni Benjamini Sitta
Mstahiki Meya wa Kinondoni Benjamini Sitta akizungumza na wananchi katika eneo hilo , amesema Tayari mipango ya Kuanza Ujenzi wa kituo hicho cha kisasa imekamilika na kuwaondoa hofu waliokuwa wakiendesha shughuli za utengenezaji magari eneo hilo kuwa watapatiwa eneo mbadala kuendesha shughuli zao.
Aidha Meya huyo wa Kinondoni amesema manispaa hiyo imeanza kuyatambua maeneo yote ya wazi na kuanza kuyaanda kwa ajili ya wafanyabiashara wote wanaofanya shughuli zao kando ya barabara kuelekea katika maeneo hayo, sanjari na kutenga fedha kiasi cha shilingi billioni moja na Nusu kwa ajili ya mikopo kwa akina mama na vijana .
Katika Mkutano huo Bw,Sitta pia alipata fursa ya kusikiliza kero mbali mbali za wananchi ikiwemo ya kupata fursa ya ajira na vibarua katika miradi mikubwa ya ujenzi ikiwemo ile ya setilite city inayojengwa chini ya usimamizi wa shirika la nyumba la taifa NHC.
Title :
Meya Benjamini Sitta atangaza neema kwa wakazi wa Kinondoni
Description : Halmashauri ya manispaa ya Kinondoni jijini Dar es salaam imetangaza kujenga kituo kipya cha kisasa cha Daladala katika eneo la Kawe maaru...
Rating :
5