Jumamosi hii rapper Joseph Haule maarufu kama Professor Jay amefunga ndoa na mpenzi wake wa siku nyingi Grace Mgonja, katika kanisa la Mtakatifu Joseph lililopo maeneo ya Posta jijini Dar es Salaam.
https://youtu.be/iwNoTy63m24
Sherehe ya ndoa hiyo imefanyika katika ukumbi wa Mlimani City, ambapo watu kibao maarufu walihudhuria pamoja na viongozi wa serikali, wabunge kutoka vyama mbalimbali hapa nchini, wasanii na wanasiasa. Miongoni mwa watu waliohudhuria sherehe hiyo ni pamoja na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, Mwenyekiti wa chadema, Freeman Mbowe, Godbless Lema, Diamond, AY, Harmonize, na wengine.
Wakati huo huo Kubwa zaidi lililoonekana kufurahiwa wageni waliohudhuria katika sherehe hiyo ni show kali iliyofanywa na AY pamoja na Diamond.
Pia Diamond aliweza kumpatia bwana harusi [Professa Jay] zawadi za kushtukiza za bidhaa zake ikiwemo maboksi matano ya Diamond Katanga, na Mankato ya Chile Perfume.