Msanii wa muziki, Professor Jay amefunga ndoa katika Kanisa la Mtakatifu Joseph la Posta jijini Dar es salaam leo Jumamosi Julai 08, 2017 na mpenzi wake wa siku nyingi Grace Mgonjo.
Kabla ya ndoa hiyo iliyoibua shangwe kwa ndugu, jamaa na marafiki waliofurika kanisani hapo, msafara wa kuelekea kanisani ulianzia nyumbani kwa Profesa Jay, Kimara-Temboni jijini Dar.
Ndoa hiyo ilifuatiwa na sherehe ya kukata na shoka iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar ambapo waalikwa walipata nafasi ya kula, kunywa hadi kusaza huku shughuli nzima ikipambwa na mahudhurio ya mastaa kibao wa Bongo.
“Namshukuru Mungu nimetimiza ahadi ya ndoa kwa mchumba wangu ambaye tumepitia mabonde na milima,” alisema Profesa Jay baada ya kutoka kanisani hapo.
Title :
Video: Professor J asema haya muda mchache baada ya kufunga ndoa
Description : Msanii wa muziki, Professor Jay amefunga ndoa katika Kanisa la Mtakatifu Joseph la Posta jijini Dar es salaam leo Jumamosi Julai 08, 2017 ...
Rating :
5