Jopo la washauri wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO), limeridhia kisiwa cha Okinoshima kilichopo nchini Japan ambacho Wanawake hawaruhusiwi kufika, kitambuliwe na kuingizwa kwenye orodha ya turathi ya Dunia .
Muonekano wa kisiwa cha Okinoshima kwa mbali
Kwa mujibu wa Gazeti la The Guardian la Uingereza limeandika kuwa Kisiwa hicho cha Okinoshima huchukuliwa kuwa kitakatifu kiasi kwamba ni wanaume pekee wanaoruhusiwa kuzuru.
Na hata wanapofika kwenye pwani ya kisiwa hicho huamliwa kuvua nguo zote na kupigwa marufuku ya kutoondoka na kitu chochote kutoka kwenye fukwe hizo.
Jopo hilo la UNESCO limekitambua kisiwa hicho kama urithi wa Dunia kwenye mkutano wake mkuu unaofanyika huko Krakow nchini Holand hii ni baada ya pendekezo lililowasilishwa mwezi May mwaka huu.
Katika kisiwa hicho, kuna madhabahu ya Munakata Taisha Okitsumiya, ambayo shughuli zake ni kutukuza Miungu wa baharini.
Gazeti la Japan Times linasema kisiwa cha Okinoshima, ni eneo maalumu ambapo hufanyika matambiko kwa ajili ya usalama wa Meli na wakazi wa Japan walitumia kisiwa hicho kuwasiliana na wakazi wa rasi ya Korea na China kati ya karne ya 19.
Miiko ya kisiwa hicho ni kama wanawake kupigwa marufuku huku Wageni wa kiume kutoka nchi za nje hutakiwa kwanza kuvua nguo zao zote na kufanya tambiko la kujitakasa kabla ya kutembelea kisiwa hicho kujionea maajabu.
Hata hivyo kwa yeyote atakayekuwa ametembelea kisiwa hicho hatakiwi kufichua chochote kuhusu waliyoshuhudia wakiwa kwenye kisiwa hicho.
Hata hivyo, bado hakuna uwezekano kwamba siku moja marufuku dhidi ya wanawake itaondolewa.
“Msimamo wetu kuhusu jinsia hautabadilika hata kama kitaorodheshwa kuwa ni Urithi wa Dunia,tutaendelea kuwadhibiti watu wanaozuru kisiwani,“amesema Meya wa Munakata Taisha wakati wa mahojiano yake na Gazeti la The Guardian.
Baadhi ya Watalii waliotembelea kisiwa hicho
Kumejengwa miundombinu pia ili kusaidia watalii kusafiri kwa urahisi wawapo kisiwani humo
Title :
UNESCO yakitambua ‘kisiwa cha maajabu’ ambacho wanawake hawaruhusiwi kufika
Description : Jopo la washauri wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO), limeridhia kisiwa cha Okinoshima kilichopo nchini ...
Rating :
5